E FM

E FM
SIKILIZA 93.7 E FM KILA SIKU

Sunday, April 20, 2014

HIZI NI DAKIKA SITA (6) ZA ALICHOSEMA 'ORDINARY' WA JAMBO SQUAD KUHUSU SHOW YAO ITAKAYOFANYIKA LEO USIKU KARATU....



Wasanii wanaounda kundi la 'JAMBO SQUAD' kutoka jijini Arusha leo wanatarajia kuperfom katika mji wa karatu katika kusherehekea sikukuu ya pasaka. 

Wasanii hao ambao ni mara yao ya pili kufanya show katika mji huo baada ya miaka kadhaa kupita, wamesema kuwa wamejipanga kuwapagawisha watu wa Karatu na viunga vyake kwa kuwaletea bonge la suprise na pia kutambulisha baadhi ya nyimbo zao mpya.
Akizungumza na sumathepresenter.blogspot.com, mmoja wa wasanii hao, Ordinary, amesema:

"...leo tutakuwa na vitu vipya zaidi tofauti na zamani. Kwa hiyo watu waje washuhudie vitu vipya pale...tutakuwa tunao ngoma kibao tutarelease pale"

Kwa upande mwingine Ordinary amesema kuwa wako mbioni kuachia video zao mpya ya nyimbo zao walizomshirikisha Dogo Janja wimbo unaojulikana kama 'Machungwa' kwa hiyo mashabiki wakae stand by kupokea mzigo mpya.
 Bofya hapa kumsikiliza Ordinary

sumathepresenter.blogspot.com pia ilizingumza na muandaaji wa show hiy, Martha ambaye pia ni mmliki wa Cannivore Pub iliyoko Karatu Mjini na kusema kuwa amejiandaa vya kutosha kuhakikisha watu wa Karatu na viunga vyake wanapata burudani siku ya leo huku akisisitiza huduma kama vinywaji na vyakula vitakuwa vikipatikana pamoja na ulinzi wa hali ya juu.

"...Kwanza waniamini nawaletea vitu vizuri, cha pili wawe na amani ulinzi upo wa kutosha watapata burudani ya kutosha, vinywaji mambo mazuri sana usiku wa leo"

Katika list ya wasanii watakao perfom siku ya leo pia ni pamoja na Contejas pamoja na Khanga moko kutoka Dar es Salaam.
Kiingilio kimetajwa kuwa ni Shilingi za Kitanzania 6000 (elfu sita tu) na show hiyo itafanyika katika ukumbi wa VIA VIA ulioko Karatu mjini.
Bofya hapa kumsikiliza Martha 

Ni ruhusa kushare ili washakaji wapate taarifa...

No comments:

Post a Comment