E FM

E FM
SIKILIZA 93.7 E FM KILA SIKU

Monday, May 11, 2015

KUHUSU PICHA CHAFU ZA SHILOLE ZILIZOSAMBAA MITANDANONI, MPENZI WAKE NUHU MZIWANDA AFUNGUKA..

MOJA kati ya story zinazotrend katika mitandao ya kijamii kwa sasa ni kuhusu kusambaa kwa picha za msanii Shilole akiwa katika show yake aliyoifanya wikiendi iliyopita nchini Ubelgiji. 


Picha hizo zinaonesha sehemu ya kifua cha msanii huyo kikiwa wazi huku maziwa yake yakiwa nje! Watumiaji wa mitandao ya kijamii wameonesha kuchukizwa na tabia za msanii huyo kuvaa nguo zinazoacha mwili wake wazi mpaka kufikia hatua ya kupigwa picha hizo. 

Akizungumza na XXL ya Clouds Fm kupitia segment ya You Heard na Soudy Brown, Shilole amesema ameshtushwa kuona picha hizo na hajapendezwa na mpigaji wa picha hizo kuzivujisha mtandaoni kwani anadai kuwa alikuwa kazini na wakati mwingine hali kama hiyo ikatokea bila yeye kujijua na kutolea mfano wa msanii wa Marekani Kanye West suruali yake kuchanika akiwa jukwaani. Akijibu swali la Soudy kuhusu kama anamuhisi mbaya wake kuvujisha picha hizo, Shilole amejibu swali hilo akidai kuwa anahisi aliyefanya hivyo ni mtu mmoja ambaye alimkatalia kufanya show yake.

Kwa upande wake Nuhu Mziwanda ambaye ni mpenzi wa Shilole ameamua kufunguka kuhusu issue hii katika mtandao wa Instagram. Cheki hapa chini:



No comments:

Post a Comment