Aliyekuwa mkuu wa jeshi nchini Misri , Abdel-Fattah
al-Sisi, ndiye Rais mpya wa Misri baada ya kushinda uchaguzi mkuu
uliofanyika wiki hii.
Muslim Brotherhood na makundi mengine yaliususia uchaguzi huo na idadi ya waliojitokeza kupiga kura inakadiriwa kuwa chini ya asilimia 45.
Hii ni licha ya kuongezwa siku ya kupiga kura, kutangazwa siku ya kitaifa ya mapumziko na hata pia kutolewa usafiri wa bure kuwapeleka wananchi kupiga kura.
Sisi alimng'oa mamlakani aliyekuwa Rais Mohammed Morsi ambaye alikuwa Rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Misri.
Chanzo: bbc
No comments:
Post a Comment