....A blog that brings you closer to all stories and news around Tanzania, Africa, and whole world at large.
Sunday, May 25, 2014
AUDIO:MSIKILIZE WAZIRI WA MIKOPO MWENGE UNIVERSITY KUHUSU KUCHELEWESHEWA MKOPO HADI WANAFUNZI WA KIKE KUJIUZA
WAZIRI wa mikopo Chuo Kikuu Cha Mwenge kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro. Bw. Cosmas Stchinga, ameamplify kuwa mpaka sasa chuo chao ni moja kati ya vyuo ambavyo havijapata malipo yao ya awamu ya nne.
Akizungumza na Suma The Presenter amesema kuwa ilitakiwa fedha ziingie tangu mwezi wa tatu mwaka mwaka huu lakini ni zaidi ya mwezi na nusu sasa hakuna dalili yeyote ya malipo.
Ameongeza kuwa, hali hiyo inasababisha wanafunzi wengi kutoingia darasani na badala yake wanaingia mitaani kutafuta shughuli za kufanya ili waweze kupata fedha za kujikimu. Kwa upande mwingine amedai kuwa imefikia hatua ya wanafunzi wa kike kwenda kujiuza katika klabu maarufu ya LA LIGA.
Pia amewaomba mawaziri wa mikopo wa vyuo mbalimbali nchini kuungana ili kuweza kutetea maslahi ya wanafunzi wa Tanzania wanaoendelea kuteseka kwa sasa na kwamba hawaihitaji kufanya migomo ili kuishinikiza bodi kutoa malipo yao.
Hali hii inakuja mara baada ya vyuo mbali mbali nchini kucheleweshewa malipo yao vikiwemo MUCCOBS na TUMAINI IRINGA.
Bofya hapo chini kumsikiliza waziri huyo
BOFYA HAPA KUMSIKILIZA WAZIRI WA MIKOPO MWUCE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment