E FM

E FM
SIKILIZA 93.7 E FM KILA SIKU

Tuesday, May 27, 2014

BREAKING NEWS: PIGO LINGINE BONGO MOVIES, MWIGIZAJI RACHEL HAULE 'RECHO' AMEFARIKI DUNIA

TAARIFA zilizotufikia hivi punde ni kuwa mwigizaji kutoka Bongo Movie Rachel Haule maarufu kama RECHO amefariki dunia. 


Kupitia akaunti ya mtandao wa Instagram, mtangazaji wa kituo cha Clouds Tv wa kipindi cha TAKE ONE, Zamaradi Mketema, ameandika kuhusiana na kifo hicho na kisha dakika chache baadae akaandika tena kuhusiana na sababu za kifo hicho.

Zamaradi amesema kuwa sabau kubwa ya kifo hicho ni kutokana na matatizo wakati wa kujifungua ambapo jana jioni mtoto mchanga wa marehemu alitangulia kufariki na kisha leo asubuhi Recho akaiaga dunia.

Mwigizaji wa Bongo Movie, Elizabeth Michael 'Lulu', nae ni mmoja kati ya wasanii wa mwanzo waliopost kuhusiana na msiba huu. Ameandika hivi:

Rachel alizaliwa mkoani Ruvuma kwenye wilaya ya Songea na kupata elimu yake katika Shule ya msing Luida iliyopo wilayani hukohoko Songea. Baada ya Muda alihamia Dar essalaam na kusoma shule ya sekondari ya Baptist iliyopo magomeni na baadaye kwenda kumalizia elimu yake ya sekondari katika Hanga. Baada ya hapo Rachel alijiunga na chuo cha magogoni kilichopo jijini Dar es salaam katika kujiendeleza zaidi kielimu.

Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi, Amen!

No comments:

Post a Comment