E FM

E FM
SIKILIZA 93.7 E FM KILA SIKU

Sunday, May 25, 2014

MAHAKAMA YAMKOSOA RAIS BANDA MALAWI


Mahakama kuu nchini Malawi imetoa hukumu dhidi ya jaribio la rais Joyce Banda kupiga marufuku matokeo ya shughuli ya uchaguzi wa urais na ubunge.


Mahakama imeiagiza tume ya uchaguzi nchini humo kuendelea na shughuli ya kuhesabu kura.
Mahakama italiangazia upya tangazo la rais Banda kwamba uchaguzi huo haufai kwa kuwa ulikumbwa na udanganyifu mkubwa.

Bi. Banda yuko katika nafasi ya pili kulinga na matokeo yaliotangazwa na kwamba ndugu ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Peter Mutharika ndio anayeongoza.

No comments:

Post a Comment