
Kamanda wa polisi mkoani hapo, Valentino Mlowola, amethibitisha tukio hilo kwa kumtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Helma Michael mwenye umri wa miaka 22. Inaelezwa kuwa mwanafunzi huyo aliuawa tarehe 13 Mei 2014 majira ya saa 4 usiku katika eneo la Nyamalango Malimbe kwa tuhuma za kuiba kompyuta ndogo za mkononi na deki. Taarifa zinasema kuwa baada ya kubainika alianza kukimbizwa na kupigwa kwa fimbo mawe na mapanga na kusababisha mauti yake.
Hata hivyo kamanda huyo amesema kuwa mwanafunzi huyo aliuawa wakati tuhuma hizo hazikuwa zimethibitishwa. Mpaka sasa watu 17 wanashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo huku kamanda Mlowola akisisitiza juu ya kutojchukulia sheria mkononi.
No comments:
Post a Comment