Serikali ya Nigeria inasema kuwa iko tayari
kuzingatia mbinu zote zitakazowezesha kuachiliwa huru salama kwa zaidi
ya wasichana mia mbili wa shule waliotekwa nyara na wanamgambo wa
kiislamu wa Boko Haram.
Awali waziri wa serikali alikuwa ameshikilia msimamo mkali kama vile kukatalia mbali pendekezo la kiongozi wa Boko Haram la kubadililishana wafungwa wa Boko Haram wanaozuiliwa na serikali na wasichana hao.
Wakati huohuo, jamaa namarafiki wa wasichana hao waliotekw anyara wameweza kuwatambua baadhi ya wasichana kutoka katika kanda ya video iliyotolewa na kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekahu siku ya Jumatatu.
Familia za wasichana hao ziliweza kutazama kanda hiyo ambapo Shekahu alisema sharti serikali iwaachilie wafungwa wao kabla ya wao kuwaachilia wasichana hao ambao kundi hilo limesema wameweza kuwasilimisha.
No comments:
Post a Comment