TAARIFA za kusikitisha kutoka katika ofisi ya serikali ya
wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni kuwa mwanafunzi mmoja aliyetajwa
kwa jina la Mwakimenya Sekabenga amefariki dunia ghafla mchana wa leo akiwa
amepumzika chumbani kwake Hall 1 Block E .
Akizungumza na Suma the Presenter, Rais wa serikali ya
wanafunzi ya Chuo hicho Bw. Filbert Nickson amethibitisha kutokea kwa kifo
hicho na kusema kuwa, mpaka sasa hakuna taarifa rasmi hasa juu ya chanzo cha
kifo hicho na kwamba tayari mwili wa marehemu umechukuliwa na kuhifadhiwa
katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili
ya uchunguzi zaidi.
Rais ameeongeza kuwa mara baada ya taratibu za hospitali
kukamilika, ofisi ya utawala wa chuo itahusika katika kusafirisha mwili wa
marehemu nyumbani kwao Morogoro sambamba na ofisi ya serikali ya wanafunzi ya
DARUSO.
Rais wa DARUSO ametuma salamu za rambirambi kwa mwenyekiti wa UDBS, Bw. Frank Mbwana, wanafunzi wa UDBS na UDSM kwa ujumla na kuwataka kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Mwakimenya Sekabenga alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili kutoka Shule ya Biashara
(UDBS) akisomea shahada ya biashara ya Uhasibu.
Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi…. Aamen
No comments:
Post a Comment