Hali hii ambayo imezoeleka kwa muda sasa imekuwa kero kwa wanafunzi chuoni hapo ambapo baadhi ya chemba zinazopitisha maji taka (maji kutoka vyooni yenye kinyesi) kufumuka na kuachwa wazi zikitiririsha maji hayo katika maeneo ambayo wanafunzi husomea au hupumzika wakisubiri vipindi.
![]() |
Chemba inayovuja maeneo ya Shule ya Sheria karibu na Academic Bridge |
Hali hii ni hatari kwa afya ya wanafunzi ikizingatiwa kuwa idadi yao ni kubwa mno na endapo magonjwa ya milipuko kama kipindupindu na homa ya matumbo (Typhoid) huweza kuleta madhara makubwa.
Inashangaza sana kwa chuo kikuu kikubwa kama hiki kinachoshika nafasi ya juu katika bara la Afrika kuwa na mazingira machafu na hatarishi kwa afya za wakazi na hata wageni.
Rai ni kwa uongozi wa Chuo na serikali ya wanafunzi (DARUSO) chini ya wizara ya Afya na Cafeteria kuchukulia uzito suala hili kwa ajili ya afya za wanafunzi wa chuo hiki.
Juhudi za kuwasiliana na utawala wa chuo na wizara ya Afya na Cafeteria bado zinaendelea na nitakujuza kadri ninavyopata taarifa.
Tazama video hapo chini kisha toa comment yako juu suala hili hapo chini....
No comments:
Post a Comment