LEO tarehe 29/06/2014 saa 12 na dakika 20 jioni ndio utakuwa wasaa wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (DARUSO -MLIMANI) ndugu Filbert Nickson kupanda ndege kutoka katika uwanja wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere International Airport (JKNI) kuelekea KOREA YA KUSINI...
Ndugu Filbert anaelekea nchini humo kuungana na viongozi wenzake wengine wa vyuo mbalimbali katika mkutano uliopewa jina TOMORROW LEADERS GLOBAL CAMP kwa ajili ya semuina ya kiuongozi ambayo inatarajiwa kufanyika kwa wiki mbili.
Akizungumza na Suma the Presenter, Rais Filbert ameeleza kuwa baada ya wiki mbili hizo viongozi wengine wakuu wa nchi mbali mbali wakiwemo wafanyakazi wa wizara mbalimbali pamoja na mawaziri wakuu watakutana kwa wiki moja ya mwisho ili kukamilisha wiki tatu.
Kwa upande mwingine ameeleza kuwa kuanzia jumatatu wanafunzi wa mwaka wa kwanza na mwaka wa pili wanatarajia kuanza mazoezi kwa njia ya matendo (FIELD) wataanza kusaini jumatatu ili kupatiwa fedha zao mapema na huku majina mengine yakitarajiwa kubandikwa mwanzoni mwa wiki hii.
Aidha amewatakia mitihani mema inayoendelea hivi sasa pamoja na kuwapa pole kutokana na mitihani hiyo huku akiwataka kuendelea kutangaza jina la UDSM huko waendako.
Msikilize hapo chini akiamplify
RAIS DARUSO AKIZUNGUMZIA SAFARI YA KOREA KUSINI PAMOJA NA MALIPO YA FEDHA ZA FIELD
No comments:
Post a Comment