
MOJA kati ya watu ambao wamepitia hali tofauti tofauti mpaka kufikia hatua ya kukata tamaa ya maisha ni pamoja na STEVEN MICHAEL a.k.a DJ BLACK ZUNGU ambaye leo hii nakuletea historia yake kwa ufupi..
Alizaliwa miaka kadhaa iliyopita katika Jiji la Arusha japokuwa wazazi wake ni wazawa wa mkoa wa Iringa. Katika kutafuta elimu, alisoma shule ya msingi katika Jiji la Arusha katika shule ya Ngarenaro na baadae kuingia sekondari katikashule ya Kisarawe iliyoko Jijini Dar es Salaam na kuishia kidato cha pili baada ya kufukuzwa shule.
Jamaa huyu anaajihusisha na shughuli za U-DJ na yeye mwenyewe anajiita 'Street DJ'. Katika mishemishe za kimaisha alishawahi kushiriki katika kinyang'anyiro cha kumsaka DJ wa TIMES FM na kushika nafasi ya pili kati ya washiriki zaidi ya 200..hii ilikuwa mwaka 2004 akiwa bado kijana mdogo sana.
Moja kati watu ambao wana mchango mkubwa kwa DJ BLACK na hatoweza kuwasahau ni Mama yake mzazi pamoja na DJ TITO. Huyu jamaa alimfundisha U-DJ pamoja na kumsaidia katika mambo mbalimbali ya kimaisha alipokuwa Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na mpenzi wake ambaye hakumtaja jina lake pamoja na CAST ambaye ndiye anaishi na kufanya naye kazi hadi sasa..
DJ BLACK amewataja MADJ wanaomfanya azidi kuipenda kazi ya UDJ kuwa ni pamoja na DJ MAFUVU wa East Africa TV na East Africa RADIO na DJ Kalonje kutoka nchini Kenya.
Jamaa amefunguka mengi sana kuhusu yeye so fanya kubofya hapo chini umsikie na ukihitaji kuwasiliana naye au kupata mixing zake mcheki kupitia YouTube kwa kuandika DJ BLACK ZUNGU, au Facebook kupitia DJ BLACK na pia unaweza kumcheki kupita 0785 976 879 au 0767 976 879
Bofya hapa kumsikiliza DJ BLACK
No comments:
Post a Comment