....A blog that brings you closer to all stories and news around Tanzania, Africa, and whole world at large.
Sunday, March 1, 2015
KUHUSU VIDEO YA BONGO HIP HOP YA FID Q.....
Freed Kubanda a.k.a Fid Q, Ngosha The Swagga Don yote yake hayo, leo usiku tarehe 1/03/2015 atakata kiu ya watanzania kwa kulipa deni aliloahidi la kuachia video ya wimbo wake unaofanya poa katika media mbalimbali nchini unaokwenda kwa jina la 'Bongo Hip Hop'.
Ngoma hiyo ambayo ilitengenezwa na producer mkongwe kwenye muziki nchini, P Funk a.k.a Majani ndani ya Bongo Records imeandaliwa na director aliyeleta mapinduzi katika utengenezaji wa video nchini hapa namzungumzia director Nisher. Kwenye uzinduzi huo ambao utafanyika katika ukumbi wa Billcanas kwa kiingilio cha 10000/= tu za Kitanzania atasindikizwa pia na wasanii kadhaa.
Fid Q ni mmoja kati ya wasanii ambao nyimbo zake nyingi huwa hatoi video lakini safari hii kaamua kulipa madeni so kama vipi fanya mpango ujitokeze pande hizo...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment