KAMA ulipata time ukasikiliza Bongo Fleva ya Clouds FM Jumamosi iliyopita, basi jina D-MALICK haliwezi kuwa geni saaana.. Ila pia kama hukusikiliza basi Suma255 inakuletea msanii mpya kabisa
kwenye game ya Bongo Fleva anayeitwa Abdulmalick Simbamgeni ambaye kisanii anajulikana kama D-MALICK.
Jamaa kashare na sisi birthday yake ambayo ni tarehe 03/03/1990 ambaye kwa sasa ni mwanachuo wa Chuo cha The Institute of Social Work akisomea shahada ya kwanza ya 'Industrial Relations'. D- MALICK kaja kwako mtanzania kwa mara ya kwanza kaachia wimbo unaoitwa 'NIPE KIDOGO' ambao umeandaliwa chini ya studio za BMK/FIDECASTRO MUSIC.
Hili ni bonge moja la ngoma of course cha kufanya ni kuidownload na kuirequest kwenye vituo mbali mbali vya redio nchini. Unaweza kuwa karibu na D-MALICK kwa kumcheki Instagram na Twitter kupitia @dmalickdreams na Facebook @ D Malick Mnyamwezi
Unaweza kudownload 'Nipe Kidogo' ya D- Malick Hapa
No comments:
Post a Comment