E FM

E FM
SIKILIZA 93.7 E FM KILA SIKU

Thursday, April 24, 2014

TUMIA DAKIKA ZAKO NNE (4) KUMSIKILIZA BWANA NOEL, MUANDAAJI WA REDD'S MISS TANZANIA WILAYA YA KARATU..


Washiriki Redd's Miss Karatu

Mwenyekiti taasisi ya T.R.Y.D.A pamoja na muandaaji wa Redd's Miss Tanzania kwa ngazi ya wilaya ya Karatu, Bw. Noel Steven, amezungumza na suma the presenter na kuzungumzia juu ya uzinduzi rasmi wa Redd's Miss Karatu 2014.


Bw. Noel amesema kuwa wamejiandaa vizuri kuhakikisha washiriki wote wanapatiwa huduma stahiki kwa muda wote watakaokuwa kambini na pia ameeleza kuwa hadi sasa wamejitokeza jumla ya washiriki tisa (9) na kusema kuwa mpaka sasa hawajatangaza zawadi atakayopatiwa mshindi bali itabaki kuwa ni 'suprise' kwa washiriki hao.

Mashindano haya pia yanatarajiwa kusindikizwa na show kali kutoka kwa Mamaa Majanga, Snura.
 
Ameongeza kuwa, bei ya tiketi ni Tsh.20,000 kawaida na Tsh.40,000 kwa V.I.P. Pia 'couple' kawaida ni Tsh. 30,000 na Couple V.I.P Tsh. 70,000  na tiketi zimeanza kuuzwa katika maeneo mbalimbali ndani ya mji wa Karatu na kusisitiza kuwa watu wachukue tiketi zao mapema. Maeneo ambayo tiketi zinapatikana ni pamoja na ofisi za T.R.Y.D.A Karatu, Kontena la Vodacom, Precious Saloon,Patamu Restaurant na Alamode store.

 Unaweza kushare story hii msikilizaji wangu.
Bofya hapa kumsikiliza Noel

No comments:

Post a Comment