BADO MUDA MFUPI TU KUFAHAMU NANI BINGWA UEFA LEO...CHEKI MASTAA BONGO WANASHABIKIA TIMU GANI LEO...TABIRI NA USHINDE HAPA HAPA PIA..
LEO kuanzia saa 3:45 usiku ndio muda utakaotegua kitendawili cha nani atakayechukua ubingwa wa bara la Ulaya (UEFA CHAMPIONS LEAGUE) ambayo fainali yake itafanyika katika mji wa Lisbon nchini Ureno.
Atletico Madrid wanashuka uwanjani wakikipiga na Real Madrid zote za Uhispania.
Tayari baadhi ya mashabiki wameanz kutabiri nani atachukua ubingwa leo usiku huku wengi wakiwapa nafasi kubwa za timu ya Atletico Madrid.
Baadhi ya mastaa Tanzania akiwemo MASANJA MKANDAMIZAJI na MADEE wameonesha pande watakapokuwa wakishabikia usiku wa leo.
MADEE amesema kuwa atashabikia Real Madrid huku MASANJA akishabikia Atletico Mardrid.
Je wewe unashabikia timu gani leo? Comment hapo chini utuambie utabiri wako na kutakuwa na zawadi kwa atakaye tabiri vizuri zaidi ikiwezekana hata na idadi ya magoli....kutakuwa na vocha ya bureee kutoka kwangu..kaa nami.
No comments:
Post a Comment