LEO CRDB wameingia kwenye headlines baada ya kutoa mabasi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) yatakayofanya safari zake kati ya Mabibo Hostel na Kampasi ya Mlimani.
Mabasi hayo ambayo yapo matatu (3) yameanza kazi rasmi leo asubuhi na yanatoa huduma pamoja na mabasi madogo mengine yaliozoeleka chuoni hapo maarufu kama "SHATO".
Taarifa zinasema asilimia 50 ya mapato itakuwa ikitumika kuwekeza ili kupata mabasi mengine yatakayomilikiwa na Chuo, asilimia 20 itaingia katika malipo ya wafanyakazi wa mabasi hayo, asilimia 20 itaingia kwenye ukarabati wa mabasi hayo na asilimia 10 itakuwa inaingia kwenye shughuli mbalimbali zinazoandaliwa kwa ajili ya wanafunzi.
No comments:
Post a Comment