E FM

E FM
SIKILIZA 93.7 E FM KILA SIKU

Saturday, May 17, 2014

NI BARCA AU ATLETICO MADRID LA LIGA LEO JIONI?

LEO jioni kitaeleweka nani bingwa katika ligi ya Hispania (LA LIGA) ambapo mahasimu wawili watakutana ili kutatua utata huo. 


Tayari Atletico Madrid wameshajiwekea nafasi kubwa ya kushinda mechi ya leo kufuatia vipigo alivyotoa kwa klabu kubwa kubwa katika ligi hiyo. 

Katika michuano ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE, mahasimu hawa walikutana katika hatua ya robo fainali na hatimaye Atletico wakawaondoa Barcelona kwa jumla ya mabao 2-1 ambapo mechi ya kwanza Barcelona wakiwa nyumbani walitoa suluhu ya mabao 1-1 na baadae katika mechi ya marudiano Atletico akiwa uwanja wa nyumbani alimbamiza Barca goli 1-0.

Atletico anatafuta sare ya aina yeyote ile ili achukue ubingwa huku tarehe 24 akitarajiwa kuingia uwanjani dhidi ya Real Madread katika fainali za UEFA zitakazofanyika LISBON.

No comments:

Post a Comment