UNAMKUMBUKA YULE MKALIMANI KWENYE MAZISHI YA MANDELA? KAPATA DILI...INGIA HAPA
Ni
jamaa ambaye dunia ilimtambua kwenye mazishi ya Hayati Mzee Nelson
Mandela mwaka jana ambaye kazi yake ilikua ni kutafsiri lugha za ishara
ambaye baadae aliinga kwa headline na vyombo mbalimbali vya habari baada
ya kufahamika hakua akipatia lugha ile ya ishara.
Thamsanqa Jantjie ndiye jina lake ambapo dunia ilimkashifu na hasa
walemavu kwa kutoa ishara zisizotafsirika kwa sasa amepata ajira baadae
Jantjie alijitetea kuwa alishikwa na kiwewe na kuona mazingaombwe wakati
wa maziko hayo.
Jantjie kwa sasa ameonekana katika tangazo la biashara akikejeli
tukio hilo lililompa umaarufu kote duniani katika tangazo hilo ambalo
linapigia debe mtandao wa kijamii wa Livelens uliotengezwa na kampuni
moja kutoka Tel Aviv Israili.
Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Max Bluvbland ameiambia BBC kuwa
Jantjie yuko timamu na kuwa alitekeleza majukumu yake bila tashwishi
yeyote ”yeye ni mtu timamu aliyepatikana na mkasa anaojutia.
Source:Bbc.
No comments:
Post a Comment