NASEEB Abdul maarufu kama Diamond Platnumz leo kupitia akaunti yake ya Instagram amepost picha akiwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Diamond yuko nchini Marekani akiendelea na show katika miji mbalimbali mara baada ya mwishoni mwa wiki hii kumaliza kufanya show yake nchini Ghana.
Rais Jakaya Kikwete yuko nchini humo kwa ziara ya kikazi na kukutana na Diamond Platnumz na kupiga picha ya pamoja ni kuonesha mchango mkubwa hasa katika kipindi hiki amabcho Diamond anashindania tuzo mbali mbali kubwa duniani ikiwemo ya KORA, MTV-MAMA na ile kubwa kabisa itakayofanyika nchini Marekani ya B.E.T
Cheki picha hapa chini....
Endelea kukaa nami kila unapopata time ya kuingia mtandaoni ili upate habari mpya kila zinaponifikia
No comments:
Post a Comment