CRISTIANO RONALDO amezua tena wasiwasi kwa mashabiki wa Ureno baada ya jana asubuhi kuonekana akitoka katika hoteli akiwa na barafu katika goti lake la kushoto huku wakijiandaa na mchezo mgumu wa kwanza dhidi ya Ujerumani.
Nyota huyo wa Real Madrid ni tegemeo katika kikosi
cha Ureno, lakini Ronaldo mwenye miaka 29 anaweza kuwakosesha raha
mashabiki kama maumivu aliyoyapata tangu akiwa katika klabu yake
yanaendelea.
Ronaldo alifanikiwa kufanya mazoezi na wachezaji wenzake kwa dakika 20 kabla ya kulazimika kutoka.
Ronaldo alionekana kusaini fulana za mashabiki kabla ya kukaa kwenye benchi akiwaacha wenzake wakiendelea.
Mshindi huyo wa tuzo ya ubora wa dunia ya ‘Ballon
d’Or 2014’ alishapumzika kwa wiki mbili kutokana na maumivu ya goti
kabla ya fainali za Kombe la Dunia.
Kurudi kwa matatizo hayo kunaweza kuwa matatizo
makubwa kwa kikosi cha Ureno chini ya kocha Paulo Bento, ambao
wanamtegemea nahodha huyo.
Inatarajiwa kuwa, Ronaldo, ambaye hata hivyo
haonekani kama anajisikia maumivu, ataanza katika mchezo wa kwanza kwa
Ureno katika fainali za Kombe la Dunia, lakini kujulikana kwa uzima wake
halisi bado tatizo.
No comments:
Post a Comment