E FM

E FM
SIKILIZA 93.7 E FM KILA SIKU

Monday, June 16, 2014

TAZAMA PICHA ZA MASHAMBULIZI YA KENYA ENEO LA MPEKETONI


Polisi nchini kenya wanasema kuwa watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabaab wamewaua takriban watu 48 kwenye mji wa mpeketoni uliopo karibu na kisiwa cha Lamu.

Watu wanne waliokuwa na silaha waliteka magari mawili na kuyaamrisha kuelekea eneo la Mpeketoni ambapo walianza kuwafyatulia watu risasi kiholela.

Walioshuhudia walisema kuwa kundi moja lilishambulia mikahawa , kituo cha polisi pamoja na kituo cha mafuta kwa saa kadhaa.
Miili ilibaki imetapakaa kila mahala huku maeneo mengine yakiteketezwa.





No comments:

Post a Comment