E FM

E FM
SIKILIZA 93.7 E FM KILA SIKU

Thursday, July 31, 2014

ANNE KANSIIME KUTUA LEO DAR


Mchekeshaji Anne Kansiime anatarajiwa kuwasili leo jijini Dar es Salaam tayari kwa burudani kali hapo August 2 kwenye ukumbi wa Golden Tulip.

Mkali wa huyo wa kuchekesha na sanaa za majukwaani Afrika Mashariki, atawasili majira ya saa kumi jioni kwa ndege ya shirika la Rwanda.
 
Anne anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari hapo Ijumaa saa tano kamili asubuhi kwenye ukumbi wa Sports Lounge uliopo Posta, na jumamosi atasalimiana na mashabiki katika viwanja vya Mlimani City.

Burudani ya hiyo ya Anne, ambayo itasindikizwa na Fredi Omondi kutoka Uganda na Pilipili wa Tanzania, huku ikinogeshwa na bendi ya ODAMA, imeandaliwa na kituo cha Radio 5.

No comments:

Post a Comment