E FM

E FM
SIKILIZA 93.7 E FM KILA SIKU

Wednesday, July 30, 2014

KAMA WEWE NI MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) NA VYUO VINGINE NCHINI NA BADO HUJAPATA FEDHA ZA 'FIELD' BASI TAARIFA YA RAIS UDSM IKO HAPA...


MOJA kati ya maswali magumu miongoni mwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam pamoja na vyuo vingine vikuu nchini Tanzania kwa sasa ni je, ni lini fedha za mafunzo kwa vitendo (Field) zitawafikia? Je, Kwa muda wote wanaosubiria fedha wataishije?

Maswali haya yamejibiwa na Rais wa Serikali ya Wanafunzi UDSM-MLIMANI Bw. Filbert Nickson mara baada ya kufanya naye mahojiano kwa njia ya simu.
Bw. Nickson amesema kuwa wao kama serikali ya wanafunzi wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kufuatilia hadi ofisi ya Waziri Mkuu (Mh. Mizengo Pinda) na kupatiwa ahadi kuwa fedha hizo zitawafikia wanafunzi wote Tanzania siku si nyingi.

Amesema kuwa ni jambo la kushangaza kwa serikali kudai haina fedha za kuwalipa wanafunzi hao wakati tayari imeshatenga Bilioni 20  kwa ajili ya kuwalipa wajumbe wa Bunge maalum la katiba huku kila mjumbe akilipwa Shilingi laki tatu (300, 000/=) kwa siku.
Aidha, Rais Nickson ameeleza kuwa bado hakuna uhakika hasa siku gani fedha hizo zitaingia kwenye akaunti za wanafunzi.

Pia, amewaomba wanafunzi wote wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam pamoja na Vyuo Vikuu vingine nchini kuwa wavumilivu kidogo huku akiwasihi viongozi wote wa vyuo vikuu nchini kufuatilia kwa umakini fedha hizo ili wanafunzi wasizidi kuumia.

Hii ni wiki ya tatu tangu kuanza rasmi kwa mafunzo kwa vitendo (field) tarehe 14/07/2014 kwa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) lakini bado wanafunzi hao hawajapatiwa fedha kwa ajili ya kujikimu pindi wawapo katika mafunzo hayo.

 Msikilize Rais wa DARUSO Bw. Fibert Nickson hapo chini kisha weka maoni yako hapo chini..

Bofya hapa kumsikiliza Rais UDSM akizungumzia kuchelewa kwa fedha za field

No comments:

Post a Comment