E FM

E FM
SIKILIZA 93.7 E FM KILA SIKU

Thursday, July 17, 2014

SIKILIZA TRUCK KUTOKA KWA AYLER FT P ICON- MSAMAHA REMIX

MOJA kati ya wasanii wanaokuja kwa kasi nchini Tanzania ni pamoja na mwanadada Irene Peter a.k.a Ayler na Paul Kevin a.k.a P Icon  ambao wote ni graduates wa elimu ya chuo kikuu..

P Icon ni mwanafunzi anayesoma shahada yake ya pili  ya Taaluma ya Lugha (Language Studies) katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ambapo mwaka jana jamaa alihitimu shahada nyingine ya kwanza 'B.A In Heritage Management and Tourism.Ayler yeye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu IFM akimalizia shahada yake ya kwanza 'Computer Science' 

Ngoma yao hii imefanywa na producer anyekwenda kwa jina la Dr. Reggy katika studio ya DM Records ambayo ipo chini ya  One Shot Music ambayo ndiyo kampuni inayowasimamia shughuli zao za muziki..

Akipiga stori mbili tatu na Suma The Presenter, P Icon amewaomba mashabiki wawapokee vizuri huku akiwaahidi vitu vizuri zaidi ambapo mwishoni mwa mwezi huu anatarajia kuachia wimbo wake mwenyewe..

Bofya hapa kusikiliza na kudownload Msamaha RMX - Ayler ft P Icon


No comments:

Post a Comment