E FM

E FM
SIKILIZA 93.7 E FM KILA SIKU

Monday, March 16, 2015

KUUNGUA KWA MABIBO HOSTEL; RAIS DARUSO ATOA TAARIFA ZA AWALI.. MSIKILIZE HAPA



Leo majira ya saa tatu asubuhi katika ghorofa ya juu kabisa ya jengo la hostel ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam (Mabibo Hostels) Block B ambalo hukaliwa na wanafunzi wa kike lilishika moto na kusababisha taharuki katika maeneo hayo hususan wanafunzi wanaoishi katika hostel hizo.

 Akizungumza na Suma The Presenter blog, Rais wa serikali ya wanafunzi ya DARUSO MLIMANI Bw. Filbert Nickson amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akitoa taarifa za awali juu ya wanafunzi anaowaongoza chuoni hapo.

Bw. Filbert Nickson amesema kuwa hakuna aliyefariki katika ajali hiyo ya moto lakini kuna majeruhi mmoja ambaye anapatiwa matibabu na pia wanafunzi wengi kuunguliwa nguo zao baada ya kuteketea kwa moto huku wengine wakipoteza vitu vya thamani kama simu na Laptop. Ameongeza kuwa hali ya usalama kwa sasa Hostel hapo ipo katika hali nzuri kwa ushirikiano baina ya polisi na polisi wasaidizi.


 Ameeleza kuwa bado chanzo rasmi cha ajali hiyo hakijajulikana lakini taarifa za awali zinasema kuwa chanzo ni hitilafu ya umeme. Ameeleza kuwa mara baada ya moto kuwaka wanafuzi walishirikiana kuuzima moto huo ndipo Zima moto na uokoaji walipofika kumalizia kuzima moto huo. 

Mpaka sasa bado haijapatikana hesabu ya hasara rasmi iliyopatikana kufuatia ajali hiyo..

Bofya hapa kumsikiliza Rais wa DARUSO MLIMANI Bw. Filbert Nickson kuhusu ajali ya moto Mabibo Hostels

1 comment: