ZIKIWA zimepita siku 12 tu na kufikisha views 97, 068 YouTube tangu kuachiwa kwake, Video ya 'Nusu Nusu' ya rapper kutoka kundi la Weusi, Joh Makini imezidi kuvunja maviza kwa
kuzidi kufanya vizuri katika kituo cha TV cha MTV BASE baada ya kuwa moja kati ya nyimbo zinazofanya vizuri katika nyimbo mpya (Best Of Spanking New). Video hiyo iliyoruka kwa mara ya kwanza katika kituo hicho zinatajwa kati ya video bora kabisa za Joh Makini alizowah kufanya.
KWA upande mwingine video ya bi dada Vanessa Mdee ambayo nayo iliachiliwa rasmi 26 March 2015 ambayo mpaka sasa imefikisha views 241, 205 YouTube imezidi kufanya poa katika kituo cha TRACE TV ambapo katika nyimbo 10 bora kutoka Africa, yenyewe imeshika nafasi ya 05.
Hii inaonesha jinsi gani muziki wa Tanzania unazidi kupasua anga za kimataifa baada ya wasanii kadhaa kutoka Tanzania wakiwemo Joh Makini, Shetta, Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz,Ali Kiba na Barakah Da Prince nyimbo zao kuonekana katika vituo vikubwa vya TV duniani.
No comments:
Post a Comment