KUPITIA kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, hit maker wa OJUELEGBA, Wizkid amefunguka kuwa hapendi kuweka maisha yake nje ya muziki kwenye vyombo vya habari.
Akijibu swali la mtangazaji wa kipindi hicho Sam Misago, Wizkid amesema kuwa ana mpenzi lakini huwa hapendi kuonekana hadharani. Sam akamtupia swali jingine je huwa haoni wivu na anakuaminije hasa unapokuwa kazini na mbali kama hivi naye akajibu huku akicheka kuwa hilo nalo ni jambo zito kiasi.
Star huyo wa hit songs kama Caro, Show You Di Money na In my Bed ameshatua Bongo jana usiku kwa ajili ya show iliyopewa jina WIZKID LIVE IN DAR inayofanyika leo katika viwanja vya Leaders Club huku akisindikizwa na wakali kutoka Tanzania wakiwemo Diamond Platnumz, Fid Q na Mfalme wa Masauti Christian Bella.
No comments:
Post a Comment