E FM

E FM
SIKILIZA 93.7 E FM KILA SIKU

Sunday, November 1, 2015

KOLABO YA DIAMOND NA WIZKID INANUKIA? ATARUDI TENA BONGO? MAJIBU YAKO HAPA!

UNAPOZUNGUMZIA mastaa wa muziki barani Afrika kwa sasa huwezi kosa kumtaja Diamond Platnumz kutoka area code +255 (Tanzania) na star wa hit song Ojuelegba wa Nigeria Wizkid.  


Sasa usiku wa tarehe 31 Oktoba 2015 wakali hao walitumbuiza kupitia stage moja katika show iliyofanyika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam. Leo asubuhi Wizkid akaandika kupitia ukurasa wake wa Istagram kumsifia Diamond kwa kuandika "Big Up to @diamondplatnumz for the love!! we link up soon!! #OneAfrica. Tayari watu wameshaanza kutabiri kuwa huenda kukawa na ujio wa ngoma kutoka kwa wawili hao. 
  Wakati huo huo Wizkid amepost pia kupitia Instagram kuwa atarudi Tanzania mwezi Desemba kwenye tamasha la FIESTA. Hii inakuja baada ya jana Wizkid kuahidi atafanya show ya bure kwa mashabiki lakini imeshindikana baada ya kukosa sehemu ya kufanyia show hiyo.

No comments:

Post a Comment