....A blog that brings you closer to all stories and news around Tanzania, Africa, and whole world at large.
Friday, February 12, 2016
UBUNGE WA PROF. JAY ULIPINGWA MAHAKAMANI. NI IPI HUKUMU YAKE? STORY NZIMA IKO HAPA
Mara baada ya uchaguzi wa October 25 mwaka 2015 kuisha, wananchi wa jimbo la Mikumi waliamua kuongeza idadi ya vichwa vikali vya Hip Hop nchini kuingia bungeni na ndipo walipomchagua Mh. Joseph Haule maarufu kama Prof. Jay aliyekuwa akigombea
kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) chini ya mwavuli wa UKAWA kuwa Mbunge wao.
Sasa aliyekuwa mgombea mwanzake kupitia Chama Cha Mapinduzi, Jonas E. Nkya aliamua kupinga matokeo hayo mahakamani. Leo majira ya jioni, Prof. Jay amepost kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa Mahakama imeamua kufuta kesi hiyo mara baada ya mlalamikaji Bw. Jonas E Nkya kushindwa kulipa gharama ya shilingi milioni 15 kama dhamana ya kesi ndani ya siku 14.
Kufuatia hukumu hiyo Prof Jay amesema kuwa kuanzia sasa yeye ni Mbunge rasmi wa jimbo hilo na pia ameishukuru timu nzima ya mwanasheria Tundu Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki ambaye alikuwa wakili katika kesi hiyo.
Isome post hiyo hapo chini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment